Home Soka Mastaa Azam Fc Waingia Kambini Rasmi

Mastaa Azam Fc Waingia Kambini Rasmi

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa kikosi cha Azam Fc tayari wameingia kambini kwa ajili ya kuanza mazoezi ya msimu mpya wa 2023/2024 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi ambapo watakaa kwa siku mbili kabla ya kwenda visiwani Zanzibar kwa kambi ya siku saba kisha kwenda nchini Morocco.

Timu hiyo inatarajiwa kukaa nchini Morocco kwa takribani wiki mbili kisha itarejea nchini ikiwa na kikosi kilicho tayari kwa ajili ya kuanza michuano ya ngao ya Jamii na kisha kuanza kampeni ya kunyakua taji la ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania pamoja na ile ya michuano ya kimataifa ambapo timu hiyo itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Katika mazoezi hayo yanayofanyika asubuhi na jioni mastaa wa kikosi hicho wakiwemo Wacolombia waliosajili msimu huu Ever Meza na Jhonier Blanco pamoja na Muivory Coast Franck Tiesse sambamba na beki Mali  Yoro Mamadou Diaby wote kwa pamoja wamehudhuria mazoezi hayo.

banner

Pia kipa Ali Ahmada naye ameungana na mastaa wa kikosi hicho baada ya kupona majeraha yake yalimfanya akafanyiwa upasuaji na kukaa nje msimu nusu msimu mzima wa ligi kuu kuanzia mwezi Januari mwaka huu na kumpisha Mohamed Mustafa aliyesajili kwa mkopo kutoka El-Merrikh ya nchini Sudan kabla ya kusajili moja kwa moja dirisha hili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited