Mastaa mbalimbali wanaocheza ligi kuu kubwa barani ulaya kama vile Mauro Icardi,Ander Herera pamoja na Jesus Vallejo wametembelea nchini kuja kutazama vivutio mbalimbali vya watalii nchini ikiwemo mbuga za serengeti na ngorongoro zilizopo nchini.
Mastaa hao wamefika nchini kwa nyakati tofauti tofauti wakija katika mapumziko wakiwa pamoja na familia zao ambapo wamekuja kutembelea mbuga hizo zenye wanyama wa aina tofauti na maajabu makubwa duniani.
Ander Herera anayekipiga katika klabu ya Paris st Germans pamoja na Jesus Vallejom wa Real Madrid wameungana na Mauro Icardi ambaye wameungana na mke wake Wanda Nara katika ziara hiyo.
Imekua kawaida kwa wageni hasa mastaa mbalimbali kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro kuja kujionea mambo mbali mbali ya kitalii mbugani hapo.