Miongoni mwa vigogo wa serikali watakaokimbia kwenye mashindano ya mbio za Kili Marathon ni waziri wa mali asili na utalii Dk.Hamisi Kigwangala na waziri wa habari ,sanaa,utamaduni na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe.
Mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager zinatarajiwa kufanyika keshokutwa Jumapili zikianzia viwanja vya ushirika mjini Moshi.
John Bayo ambaye ni mjumbe wa kamati ya mbio amesema kuwa waziri Kigwangala ndiye atakayekuwa mgeni rasmi na mwenyeji wake akiwa Dk. Mwakyembe.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa upande wa maandalizi upo hatua ya mwisho ambapo usajili utafungwa kesho saa 6:00 mchana na askari 310 tayari wameshaandaliwa kwa ajili ya kuimarisha usalama barabarani wakati wa mbio hizo.