Home Makala Maximo Atua Kmc

Maximo Atua Kmc

by Dennis Msotwa
0 comments
Maximo Atua Kmc-Sportsleo.co.tz

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo ametambulishwa leo kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya KMC Fc akichukua mikoba ya Kally Ongala aliyetupiwa virago mwezi Mei kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo.

Kocha aliyejipatia umaarufu hapa nchini miaka ya 2007 amejiunga na Kmc ambapo mapema hii leo ametambulishwa na klabu hiyo mbele ya waandishi wa habari.

banner

Kocha huyo anayejulikana kwa misimamo mikali na kupenda nidhamu kwa mastaa wa klabu anayoifundisha anatarajiwa kuleta mabadiliko chanya klabuni hapo.

Lengo kuu la mabosi wa Kmc ni kuimarisha nidhamu ambayo itapelekea timu hiyo kufanya vizuri uwanjani hasa kwenye michuano ya ligi kuu na kombe la Shirikisho la Crdb nchini.

Maximo (63) raia wa Brazil ambaye pia amewahi kuinoa Young Africans Sc anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited