Kocha wa zamani KMC Jackson Mayanja apata mrithi wake Haruna Harerimana aliyesainishwa kunoa kikosi hicho kwa kandarasi ya mwaka mmoja na miezi nane.
Jackson Mayanja alisitishiwa mkataba wake baada ya bodi ya KMC kuona timu kutokuwa na matokeo mazuri kwenye ligi na kimataifa.
Mwenyekiti wa bodi ya KMC amesema ana imani na Haruna Harerimana atarudisha morali na hali ya kujiamini kwa timu kwani ameshaanza kazi ya kuinoa kwa ajili ya mmashindano ya ligi kuu na kombe la shirikisho Azam.
Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa kombe la Azam.