Kocha wa klabu ya Mbeya kwanza Mbwana Makata na meneja wa klabu hiyo David Naftari wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitano kufuatia kuwashawishi wachezaji kugomea mchezo dhidi ya Namungo ambao ulipangwa kufanyika mkoani Lindi katika uwanja wa Ilulu.
Katika mchezo huo gari la wagonjwa lilichelewa kwa dakika 24 ambapo ilitakiwa mchezo uanze baada ya gari hilo kufika kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ambapo mchezo unaweza usiendelee endapo gari la wagonjwa litachelewa kwa nusu saa hivyo kamati iliwakuta wahusika na kosa la kukiuka kanuni ya 32:7 ya ligi kuu kuhusu kuvuruga mchezo.
Licha ya viongozi hao kufungiwa miaka mitano pia klabu ya Mbeya kwanza imepoteza mchezo huo ambapo Namungo Fc wamepewa alama tatu na magoli matatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.