Home Makala Mayele Atetema Tena

Mayele Atetema Tena

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kutofunga kwa takribani mechi nne mshambuliaji Fiston Kalala Mayele amefanikiwa kufunga bao la 13 la ligi kuu msimu huu na kumfikia George Mpole wa Geita Gold SC ambaye alikua kinara wa mabao.

Mayele alifunga bao hilo dakika ya 34 katika mchezo dhidi ya Mbeya kwanza FC akiunganisha krosi ya Salum Abubakari ambaye aliwahadaa walinzi na kupiga krosi ya bao hilo ambalo Mayele alifunga kwa kichwa.

Katika mchezo huo Yanga sc jumla iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 huku ikifikisha jumla ya alama 63 katika michezo 25 ya ligi kuu huku ikisaliwa na michezo 5 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited