Home Makala Mayele,Baraza Wang’ara Tuzo Januari

Mayele,Baraza Wang’ara Tuzo Januari

by Dennis Msotwa
0 comments

Mchezaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Kalala Mayele ameng’ara katika tuzo za wachezaji bora wa ligi kuu nchini baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi januari huku Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza akishindia tuzo ya kocha bora.

Tuzo hizo hutolewa na kamati maalumu ya tuzo iliyopo katika Bodi ya ligi kuu nchini ambapo Mayele amewashinda Reliants Lusajo wa Namungo Fc na Tepsie Evance wa Azam Fc ambapo Mayele aliisaidia Yanga sc kushinda dhidi ya Coastal Union akishinda bao moja huku akitoa pasi ya bao dhidi ya Polisi Tanzania.

Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza yeye ameibuka kocha bora wa mwezi januari akiwashinda Nasredine Nabi na Mathias Rule wa Mbeya City ambapo aliingoza kushinda michezo miwili ikiwemo mchezo dhidi ya Simba sc na kutoa sare mchezo mmoja dhidi ya Biashara united.

banner

Awali mwezi disemba tuzo hizo zilikwenda kwa Reliants Lusajo wa Namungo Fc na Kocha Melis Medo wa Coastal Union.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited