Kocha mkuu wa Simba Sc Sven Vanderbroeck amewekwa kitimoto na mabosi wa klabu hiyo kutokana na kutokufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika timu kwani haileti msisimuko kama awali kwa mashabiki.
Sven anahesabiwa siku tu katika kikosi cha Simba iwapo hatakubali kurekebisha dosari zake katika timu inayoongoza nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 50.
Mabosi wa Simba walianza msako wa kumtafuta kocha mwingine ambapo walimpendekeza kocha wao wa zamani Goran Kopunovic lakini tayari alishachukuliwa kufundisha timu nyingine Eritrea.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.