Home Makala Mbelgiji Yanga Ashusha Morrison Mwingine

Mbelgiji Yanga Ashusha Morrison Mwingine

by Sports Leo
0 comments

Wakati   Bernard Morrison mchezaji wa Yanga akiendelea kuwafanya wapenzi wa timu hiyo washindwe kuamini anachofanya uwanjani baada ya kuhaidi kuifanyia maajabu timu hiyo  Luc Eymael ambaye ni kocha mkuu wa Yanga  ameshusha kifaa kingine jijini kimyakimya raia wa Ghana, Joseph Quansah.

Quansah mwenye umri wa miaka 29 ametokea katika klabu ya Amodaus Professional na tayari ameshamwaga wino kuichezea Yanga miaka miwili ana uwezo katika dimba la kati  huku  akiwa na vionjo kama vya mtangulizi wake Morrison.

Habari njema kwa Wanayanga ni kuwa kocha wao Eymael ameahidi kukamilisha idadi yake kwa kushusha mchezaji mwingine ili kufikisha idadi ya watatu anaowahitaji kikosini na anajua sehemu atakayowatoa wachezaji hao kwa kuwaalishindwa kuwasajili dirisha dogo baada ya kuchelewa kutua nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited