Klabu ya Simba sc imefanikiwa kukamilisha mazungumzo na kocha wa Vipers Fc ya nchini Uganda Mbrazil Roberto Oliviera aka Robertinho kuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Zoran Maki ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa faida ya pande mbili.
Robertinho amekaa Vipers tangu mwezi augusti mwaka uliopita akichukua nafasi ya kocha Fred Kajoba tayari amekubakiana kila kitu na Simba sc huku akilazimika kuvunja mkataba wake na Vipers wa miaka miwili uliosalia klabuni hapo.
Kocha huyo pia ametaka kuja na msaidizi wake Marcelo Cardoso kuja kumsaidia klabuni hapo huku nafasi ya Juma Mgunda ama Selemani Matola itakua shakanim kuendelea kukaa klabuni hapo japo Matola ndio anaweza kuondoka akamuacha Mgunda kama kocha msaidizi namba mbili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Taarifa kamili za kocha huyo kujiunga rasmi na klabu bado hatujazipa japo inasemekana kwa sasa anaweza kutua mwezi Desemba wakati wa dirisha dogo ambapo timu itaendelea kubaki chini ya Juma Mgunda.