Lionel Messi ambaye ni mchezaji namba moja aliyeifungia mabao mengi Barcelona amerejea mazoezini jana baada ya jaribio lake la kulazimisha kuondoka kushindikana.
Kufika kwa muargentina huyo na kufanya mazoezi inakuwa ni mara ya kwanza tangu kuwasili kwa meneja mpya wa klabu hiyo,Ronald Koeman.
Barcelona itakuwa na mechi ya kwanza Septemba 27 ambapo itachuana vikali na Villarreal kutoka La liga.