Home Makala Mexime Atimuliwa Kagera Sugar

Mexime Atimuliwa Kagera Sugar

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Kagera Sugar Fc imeachana na kocha wake Mecky Maxime kwa makubaliano ya pande mbili siku moja baada ya timu hiyo kupokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Azam Fc katika ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania.

Mexime alijiunga na klabu hiyo msimu huu lakini klabu hiyo imekua na matokeo yasiyoridhisha ambapo mpaka sasa ipo katika hatari ya kushuka daraja ikiwa katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu nchini.

banner

Mbali na Kocha Maxime, Kagera pia imetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wa viungo, Francis Mkanula ambapo kwa  mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Marwa Chambari katika kipindi hiki cha mpito.

Sasa Kagera Sugar inayomilikiwa na kampuni ya sukari nchini haina budi kurudi tena sokoni kutafuta mwalimu wa kuinoa timu hiyo pamoja na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo kikosini humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited