Home Soka Mexime Atua Dodoma Jiji

Mexime Atua Dodoma Jiji

by Sports Leo
0 comments

Aliyekua kocha wa Ihefu Fc(Sasa Singida Black Stars) Mecky Mexime ametua rasmi katika klabu ya Dodoma Jiji Fc kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa msimu wa ligi kuu wa 2024/2025 ambapo tayari klabu hiyo imemtangaza rasmi hii leo.

Mecky aliachana na Singida Black Stars ambayo aliitumikia msimu uliopita wa ligi kuu ya soka ya Nbc na kuisadia kumaliza katika nafasi ya saba ikiwa na alama 36 katika michezo 30 ya ligi kuu ya soka ya Nbc nchini Tanzania bara na klabu hiyo tayari imemuajiri Patrick Aussems kama kocha mkuu.

Mecky kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Kagera Sugar anachukua nafasi ya John Baraza ambaye ameachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande mbili ambapo ameiacha klabu ikimaliza msimu katika nafasi ya 12 ya msimamo ikiwa na alama 33.

banner

Kocha Mecky ana kazi kubwa ya kufanya ambapo ataanza na usajili wa mastaa mbalimbali kikosini humo huku pia akitakiwa kuwatema wale ambao ataona hawahitaji kikosini humo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited