Kocha wa klabu ya Simba sc Juma Mgunda ametwaa tuzo ya Kocha bora wa mwezi Mei baada ya kuwashinda Kocha wa Yanga sc Miguel Gamondi na kocha wa Azam Fc Bruno Ferry ambapo kocha ameifanya klabu yake kuvuna alama nyingi zaidi kwa mwezi huo.
Mgunda alivuna jumla ya alama 19 katika michezo saba aliyocheza klabu yake ya Simba sc ikivuna alama tatu katika michezo sita huku ikipata sare katika mchezo mmoja na kuifanya klabu hiyo kumaliza ligi kuu katika nafasi ya tatu na kukata tiketi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Kati mechi hizo sita ambazo Simba sc ilishinda imo ambayo aliiongoza kuifunga Azm Fc kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kinyume na matarajio ya wengi kuwa Simba sc ingepoteza mchezo ule kwa idadi kubwa ya mabao kutokana na kutokua na kiwango kizuri huku ikiwakosa mastaa kibao kikosini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mgunda amekua akitumika klabuni hapo kama kocha wa muda baada ya makocha wakuu kutimuliwa mara kwa mara hali iliyozua maswali kuhusu hatma yake klabuni hapo ambapo alijiunga akitokea Coastal Union japo amekua na mchango mkubwa akishika timu kama kocha mkuu.