Site icon Sports Leo

Miloud Atua Ismailia

Kocha wa Yanga sc Miloud Hamdi amejiunga na timu ya Ismailia ya nchini Misri baada ya kumaliza mkataba na klabu hiyo ya Jangwani mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu nchini.

Kocha huyo ameondoka Yanga sc baada ya mkataba wake kutamatika mwezi huu na mabosi wa klabu hiyo hawajaonyesha nia ya kumuongeza licha ya kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji matano msimu.

Miloud ameondoka pamoja na wasaidizi wake wawili kocha msaidizi pamoja na kocha wa viungo na kuwaacha kwenye mataa viongozi wa Yanga sc ambao walikua wamegawanyika kuhusu kumpa mkataba kocha huyo.

Miloud alijiunga na Yanga sc akitokea Singida Black Stars alikodumu mwezi mmoja pekee kisha kuja Yanga sc ambapo ameifundisha kwa takribani miezi mitano pekee na kuipa makombe matatu ya ligi kuu,Kombe la Shirikisho na Muungano.

Ismailia imempa kocha huyo mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza tena mmoja na itampa mshahara mara mbili ya ule aliokua analipwa Yanga sc.

Exit mobile version