Mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga, Shija Richard Shija ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote katika klabu ya Yanga Sc baada ya sakata la GSM kujiengua na ofa zilizopo nje ya mkataba.
“Nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ,Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote .Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote”alisema Shija
Aliongeza kwa kusema ukweli hata usipousema huwa una tabia ya kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele.