Kaimu kocha mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema kuwa kwa sasa hajui hatma yake tangu nafasi ya Mwinyi Zahera kuchukuliwa na Mbelgiji Luc Eymael.
Tumefurahi ujio wa kocha mpya ndani ya Yanga na tunatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anafanya kazi vizuri kwa kumuelekeza utaratibu wote wa timu.
“Kwa upande wangu bado sijajua hatma yangu viongozi ndio wanaojua na ndio wenye majibu kuhusu uwepo wangu ndani ya timu ,kwa sasa bado naendelea kukinoa kikosi hadi kocha mpya atakapokabidhiwa rasmi kikosi”alisema Boniface Mkwasa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.