Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kiko timamu kwa asilimia 100 kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba
Mchezo huo utapigwa leo saa 11 jioni kwenye uwanja wa Taifa
Akizungumza baada ya mazoezi ya mwisho jana, Mkwasa alisema hana wasiwasi kuelekea mchezo huo, ari ya vijana wake iko juu
“Kikosi kimekamilika, wachezaji wako vizuri na ari ya ushindi iko juu, tumekamilisha maandalizi yetu kwa 100% dhidi ya Simba. Tunasubiri dakika 90,” alisema
Mchezo huo wa kwanza wa dabi msimu huu, una umuhimu wa kipekee kwa Yanga ambayo imesukwa upya
Wakiwa nyuma ya wapinzani wao kwa tofauti ya alama 10 na michezo miwili mkononi, kwa Yanga kupoteza mchezo huu hayatakuwa matokeo mazuri katika kampeni yao ya kurejesha ubingwa wa ligi kuu ambao wameupoteza kwa misimu miwili sasa
Leo Yanga itawasoka beki Lamine Moro anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano na mshambuliaji Tariq Seif ambaye alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United
Aidha ujio wa Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi na Yikpe Gnamien umeongeza makali ya safu ya ushambuliaji
Wachezaji hao wamekuwa wakifanya vizuri mazoezini na pengine leo huenda wakapewa nafasi ya kuanza