Winga wa klabu ya Yanga sc Jesus Moloko Ducapel amefanyiwa upasuaji mdogo wa goti la kulia kutokana na kupata majeraha siku kadhaa zilizopita katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Biashara United na kutolewa nje kipindi cha kwanza.
Moloko mwenye mchango mkubwa katika kikosi cha Yanga akichangia kwa mabao 3 na pasi za mwisho 3 atakua nje ya uwanja kwa kipindi kifupi kwa mujibu wa taarifa kutoka klabuni hapo.
Nafasi ya winga huyo mwenye nguvu itakwenda kuzibwa na Dennis Nkane pamoja na Chico ushindi ambaye amerejea kutoka katika majeraha huku winga Deus Kaseke nae akileta upinzani kuwania nafasi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.