Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewapumzisha mastaa wake kwa muda akiwepo Nchimbi,Morrison na wachezaji wengine chini ya uangalizi mkali huku akiwapa maagizo ya kuyatekeleza kipindi hiki baada ya agizo la serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa mwezi wa mmoja ili kupambana na Corona.
Eymael amewapa ratiba kila mmoja ya kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayopaswa kufanya ukiwepo na ratiba ya chakula wanachopaswa kula wakiwa majumbani kwao na endapo hawatakela watakuwa kwenye wakati mgumu.
“Wachezaji wote na viongozi wa benchi la ufundi la Yanga tunapaswa kuwa makini kujikinga na virusi vya Corona ,pia nitazidi kuwasiliana na kila mchezaji kupitia njia ya video ya watsapp ili kujua maendeleo yao kwenye maagizo ambayo nimewapa”alisema
Kocha huyo anatarajia kurudi kwao Ubelgiji siku ya alhamisi ikiwa mambo yatakuwa vizuri ili akafurahi na familia yake kwa kipindi hiki cha mapumziko.