Kocha mkuu wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho ameamua kumuaga mchezaji wake Christian Eriksen kwa kumtaka aondoke akiwa na furaha kwani mara kwa mara tetesi zilikuwa zikitajwa kuwa anataka kuondoka kwenye timu hiyo kwenye usajili wa Januari.
Christian Eriksen alionekana juzi akiwaaga wachezaji wenzake na mashabiki wa timu hiyo wakati Spurs ilipokuwa ikicheza na Middlesbrough kwenye mchezo wa kombe la FA pia kumpatia shabiki jezi yake aliyoitumia kwenye mchezo huo.
“Nafikiri anatakiwa kuondoka hapa akiwa na furaha ,ni mchezaji mkubwa ,mtiifu akiwa mazoezini pia amekuwa akionyesha kiwango cha juu sana kwenye kila mchezo”alisema Jose Mourinho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Eriksen anatarajiwa kuondoka kwenye timu hiyo na kujiunga na Inter Milan kama iliyosemekana walikuwa wakimuhitaji mchezaji huyo.