Home Soka Mpanzu Kuanza na Kengold Fc

Mpanzu Kuanza na Kengold Fc

by Dennis Msotwa
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Ellie Mpanzu ataanza kuichezea klabu hiyo rasmi Disemba 18 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kengold Fc utakaofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mpanzu ambaye alisajiliwa tangu mwezi Oktoba lakini klabu hiyo ilishindwa kumuingiza kwenye mfumo mpaka Disemba 15 dirisha dogo la usajili lilipofunguliwa ambapo amechukua nafasi ya Ayoub Lakred.

Tayari jina la kiungo mshambuliaji huyo lipo kwenye mfumo na leseni yake imeshapatikana sasa kinachosubiliwa ni uamuzi wa kocha Fadlu Davis kumuanzisha ama la ambapo kwa zaidi ya asilimia tisini ana uhakika wa kuanza kutokana na kushiriki mazoezi muda mrefu.

banner

Mpanzu anatajwa kama usajili utakaokwenda kuibadili Simba sc katika eneo la ushambuliaji ambapo ataongeza nguvu kutokana na kuwa na uwezo wa kucheza nafasi zote za eneo la mbele.

Simba sc mpaka sasa ina alama 28 ikiwa inecheza michezo 11 ya ligi kuu nchini ambapo inatarajiwa kuibuka na ushindi mnono katika mchezo huo dhidi ya Kengold Fc iliyomkiani mwa ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited