Yanga bado inajiuliza kuhusu kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Nkana Fc ya nchini Zambia Idriss Mbombo kutokana na mshambuliaji huyo kuhitaji mshahara wa kufuru.
Inadaiwa tayari makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili klabuni hapo Eng.Hersi Said amezungumza na staa huyo lakini kikwazo kikubwa ni mshahara wa dola elfu kumi anaohitaji mshambuliaji huyo ndio unawapa kigugumizi mabosi wa jangwani kwani ni mshahara ambao analipwa kocha Cedrick Kaze.
Ikiwa dili hilo litashindikana basi timu hiyo itaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Rangers ya Ufaransa Ferebory Dore.