Unamkumbuka mshambuliaji wa zamani wa Simba sc na Kagera sugar?ambaye alitamba kisha akasajiliwa Azam fc?
Baada ya kuwa nje ya dimba takribani mwaka mmoja akiuguza majeraha ya goti, mshambuliaji wa azam fc Mbaraka Yusuph, amejumuika na wenzake mazoezini leo Jumapili baada ya kupona majeraha ya goti.
Yusuph alifanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia Aprili mwaka jana katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini, kufuatia kubainika kuchanika mtulinga wa kati wa goti hilo (Anterior Cruciate Ligament Tear).
Licha ya kusahaulika kutokana na majeraha bado Mbaraka sio mshambuliaji wa kubeza hasa anapokua na utimamu wa mwili.