Home Makala Mtibwa Mabingwa Mapinduzi Cup

Mtibwa Mabingwa Mapinduzi Cup

by Sports Leo
0 comments

Timu ya  soka ya Mtibwa Sugar imeibuka mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Simba sc kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Aman Zanzibar.

Simba licha kuongozwa na wachezaji mastaa wakiwemo Meddie Kagere na Clotous Chama walijukuta wakiruhusu bao dakika ya 38 likifungwa na Awadh Salum kufuatia uzembe wa mabeki kushindwa kuokoa mpira uliozagaa.

Licha ya kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar Simba ilishindwa kupata bao huku beki iliyokuwa na Erasto Nyoni,Tairon Da Silva,Gadiel Michael na Haruna Shamte ilishindwa kuendana na kasi ya washambuliaji wa Mtibwa walioongozwa na Jafarry Kibaya na Salum Kihimbwa na mpaka dakika 90 zinakamilika Simba waliukosa ubingwa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited