Timu ya soka ya Mtibwa Sugar imeibuka mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Simba sc kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Aman Zanzibar.
Simba licha kuongozwa na wachezaji mastaa wakiwemo Meddie Kagere na Clotous Chama walijukuta wakiruhusu bao dakika ya 38 likifungwa na Awadh Salum kufuatia uzembe wa mabeki kushindwa kuokoa mpira uliozagaa.
Licha ya kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar Simba ilishindwa kupata bao huku beki iliyokuwa na Erasto Nyoni,Tairon Da Silva,Gadiel Michael na Haruna Shamte ilishindwa kuendana na kasi ya washambuliaji wa Mtibwa walioongozwa na Jafarry Kibaya na Salum Kihimbwa na mpaka dakika 90 zinakamilika Simba waliukosa ubingwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.