Uongozi wa klab ya Mtibwa sugar umefikia maamuzi ya kuachana na Aliyekuwa kocha wao Mkuu Habib kondo baada ya kuwa na mwenendo usio ridhisha kikosini humo hasa katika michuano ya ligi kuu nchini.
Mpaka sasa timu hiyo katika michezo mitano ya ligi kuu haijafanikiwa kuibuka na ushindi wowote ambapo imepata sare mbili huku ikipoteza michezo mitatu na kuifanya iwe katika hatari ya kushuka daraja mkiani mwa msimamo wa ligi kuu.
Kutokana na kutimuliwa kwa kocha huyo sasa timu hiyo itakua chini ya kocha msaidizi Awadh Juma mpaka pale kocha mkuu atakapopatikana huku kukiwa na tetesi za kurejeshwa kwa kocha Zubeiry Katwila ambaye wiki iliyopita alijiuzuru kuifundisha timu ya Ihefu Fc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Katwila alikua kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar mpaka alipoamua kuachia ngazi na kujiungana na Ihefu Fc msimu wa 2021 na sasa anatajwa kurejea klabuni hapo ambapo pia anahusishwa na kujiunga na Singida Fountain Gate Fc.