Home Makala Mtibwa Sugar Yaonja Ushindi

Mtibwa Sugar Yaonja Ushindi

by Sports Leo
0 comments

Mtibwa Sugar ikiwa chini ya kocha wake Mpya  Zubeir Katwila imeichapa Geita Gold kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Oktoba 26, kwenye uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro.

Ushindi unakua wa kwanza kwa timu hiyo tangu msimu wa ligi uanze na umewafanya sasa kufikisha alama tano katika michezo saba ya ligi kuu ya Nbc inayoendelea hapa nchini ambapo pia sasa wamesimama katika nafasi ya 13.

Ladack Chasambi alifunga bao la uongozi dakika ya 20 ya mchezo huku Seif Karihe nae akifunga mabao mawili dakika za 49 na 58 na kulizamisha jahazi la Geita ambao walipata bao la kufutia machozi dakika ya 83 baada ya Mohamed Makaka kujifunga.

banner

Mtibwa sugar imeanza kuona matunda baada ya kubadili benchi la ufundi wakimrudisha mwalimu Katwila baada ya kuachana nae tangu mwaka 2020 ambapo alijiunga na Ihefu Fc.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited