Home Soka Mustapha Kusalia Azam Fc

Mustapha Kusalia Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Mlinda mlango wa kimataifa wa Sudan Mohamed Mustapha sasa rasmi amekamilisha Uhamisho wake wa moja kwa moja Kujiunga na klabu ya Azam Fc akitokea klab ya Al Marreikh Fc ya nchini Sudan baada ya makubaliano baina ya vilabu hivyo kufikiwa.

Mohamed Mustapha alijiunga klabu ya Azam Fc kwa mkopo wa miezi sita tu (kipindi cha dirisha dogo la Usajili la mwezi januari 2024) kuchukua nafasi ya Ali Ahmada na Abdulai Iddrisu ambao walikumbwa na majeraha makubwa yaliyowalazimu kukaa nje kwa miezi zaidi ya sita baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kipa huyo baada ya kutua Chamazi alionyesha kiwango kizuri ambapo ameisaidia timu hiyo kumaliza ligi kuu nchini katika nafasi ya pili kiasi cha klabu hiyo kuamua kumsajili moja kwa moja licha ya klabu yake kumhitaji kurejea nchini Sudan.

banner

Usajili huo mpaka sasa upo katika hatua za mwisho kukamilika huku mabosi wa klabu hiyo wengi wao wakikoshwa zaidi na kiwango cha kipa huyo katika mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho la Crdb dhidi ya Yanga sc Visiwani Zanzibar ambapo staa huyo alidaka vizuri katika dakika tisini na akicheza penati mbili wakati wa mikwaju ya matuta.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited