Beki tegemeo wa klabu ya Yanga sc na Taifa Stars Bakari Mwamnyeto amesaini mkataba wa miaka miwili kusalia klabuni hapo baada ya ule wa awali kumalizika msimu huu.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga sc zinasema kwamba beki huyo amesaini mkataba huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 200 za kitanzania na kuzima tetesi za kuondoka klabuni hapo hasa alipokua akihusishwa na klabu ya Simba sc.
Yanga sc ilimsajili Mwamnyeto misimu miwili iliyopita akitokea Coastal Union ambapo amefanikiwa kuonyesha kiwango bora kabisa na kupewa unahodha wa klabu hiyo mbele ya mastaa kama Fiston Mayele na Yannick Bangala Litombo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.