Home Makala Mwamnyeto Kuwakosa Al Merrekh

Mwamnyeto Kuwakosa Al Merrekh

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga imetoa taarifa rasmi kuwa nahodha wa kikosi chao Bakari Mwamnyeto hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kesho kuelekea Rwanda kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh.

Mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Pele Nyamirambo nchini humo ambapo Yanga sc atakua mgeni huku ikithibitishwa rasmi kuwa beki huyo ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia hivyo hatosafiri na timu.

Mwamnyeto amekua ni mchezaji muhimu hasa katika michuano ya kimataifa kutokana na uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi huku pia akiwa vizuri kucheza na kuokoa mipira ya juu.

banner

Licha ya kutokuwepo kwa nahodha huyo badao kocha Miguel Gamondi ana machaguo kadhaa eneo la ulinzi akiwa tayari anao Dickson Job na Ibrahim Hamad ambao wamekua wakicheza vizuri katika nyakati nyingi klabuni hapo.

Yanga sc wataivaa Al Merrikh katika mchezo huo utakaofanyika siku ya jumamosi saa kumi jioni kwa saa za nyumbani nchini Tanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited