Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili beki na nahidha wake Bakari Mwamnyeto baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa staa huyo huku kukiwa na maboresho makubwa ya fedha ya kusainia mkataba huo.
Mabosi wa Yanga sc wanamuona beki huyo akiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kikosi hicho sambamba na mabeki wenzake Ibrahim Bacca na Dickson Job hivyo kumuacha ni sawa na kuachia silaha ya ushindi vitani.
Tayari mkataba huo umeshasainiwa na sasa kilichobaki ni kutambulishwa pekee huku tetesi za kuwa anatakiwa na klabu ya Simba sc zikiwa zimezimwa tayari kutokana na dili hilo kukamilika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mwamnyeto kwa miaka mitatu amekua ni nahodha mwenye mafanikio zaidi nchini akibeba mataji ya ligi kuu na kombe la shirikisho mara tatu huku akipata mafanikio zaidi tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Coastal Union mwaka 2020.