Klabu ya JKT Tanzania ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha usajili wa kiungo James Mwashinga kutoka katika klabu ya Pamba Jiji Fc ambae mkataba wake umeisha klabuni hapo.
Mpaka sasa kuna vita Kubwa sana ya kumnasa kiungo huyo fundi ambae alikuwa na msimu bora sana na wanalindanda akicheza maeneo muhimu ya ulinzi na kiungo.
Mbali na Jkt Tanzania pia klabu za KMC na Tabora United zote zinahitaji huduma ya Mwashinga huku JKT Tanzania ikipenya moja Kwa moja mstari wa mbela kutokana na ofa walizoweka mezani Kwa Mwashinga.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia bado Pamba Jiji Fc inamuhitaji kiungo huyo kusalia klabuni hapo ambapo amekua na faida kubwa kiufundi akicheza kama mshambuliaji wa pili sambamba na nafasi zote za kiungo pamoja na beki wa kati.