Mwendelezo wa ligi kuu Tanzania Bara utaanza kwa Yanga na timu nyingine zenye mechi za viporo na kwa upande wa Robo fainali ya FA itachezwa punde baada ya mechi za viporo kumalizika.
Ligi itachezwa kwa muda wa mwezi mmoja na kwa siku zitachezwa mechi tano saa 8,10,12 na saa 2 usiku ambapo mbili zitacheza uwanja wa Chamazi, mbili nyengine Uhuru na Uwanja wa Taifa mechi moja.
Wadhamini wa Ligi watachangia fedha kidogo sana ila upande wa timu zitajigharamia kwa asilimia kubwa sehemu za maradhi na chakula watakapokuwa Dar, kwa kipindi chote cha kumalizia Ligi ambapo kila baada ya raundi moja kumalizika kutakuwa na mapumziko ya siku mbili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.