Home Makala Nahodha Wa Watford Agoma Kurejea Kambini

Nahodha Wa Watford Agoma Kurejea Kambini

by Sports Leo
0 comments

Nahodha wa klabu ya Watford, Troy Deeney amesema kuwa hataweza kuripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo kutokana na hofu ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

Wachezaji wengi wa Watford pamoja na viongozi wa klabu hiyo  wamegomea kurejea rasmi kambini kuanza mazoezi ya pamoja baada ya kupata ripoti kuwa wachezaji wenzao watatu wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona hii ni baada ya kufanyiwa vipimo ikiwa ni maandalizi ya kurejea kwa Ligi Kuu England.

Ripoti zinaeleza kuwa wachezaji wengi wamejiunga na Deeney baada ya kuweka bayana mpango huo ,huku wale ambao wamekutwa na maambukizi wakitwengwa kwa muda wa siku saba karantini ili kuwajulia hali yao itakavyokuwa na wasiweze kuwaambukiza wengine.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited