Namungo Fc ya Lindi imeamua kumalizana na mchezaji kutoka Lipuli Fc,Fredy Tangalo ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha.
Huu ni usajili wa kwanza kwa Namungo Fc inayonolewa na kocha mkuu, Hitimana Thiery ambaye anawania tuzo ya kocha bora kwa msimu wa 2019/20.
Namungo inaimarisha kikosi chake kwa sasa kwa ajili ya msimu ujao ambapo imepata nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho na kukutana na bingwa wa ligi Simba.