Home Makala Ndala Atua Kmc Fc

Ndala Atua Kmc Fc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Issa Ndala amejiunga na klabu ya Kmc kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima baada ya klabu yake ya Azam Fc kumsajili Yannick Bangala kutokea Yanga sc hivyo kuhitajika kupunguza mchezaji mmoja wa kimaifa ili kuendana sawa na kanuni za ligi kuu nchini.

Ndala ambaye alisajiliwa kutokea Plateau United ya nchini Nigeria ameitumika klabu ya Azam fc kwa misimu takribani miwili na hatimaye msimu huu kocha Yousouph Dabo ameonyesha kutokua na imani naye na kukubali usajili wa Bangala kutua klabuni hapo.

Tayari klabu ya Kmc imetangaza usajili wa kiungo huyo kwa mkopo wa msimu mzima na tayari ameshajiunga na kambi ya maandalizi ya klabu hiyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited