Home Makala Neymar Atemana na Waarabu

Neymar Atemana na Waarabu

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Neymar Dos Santos yupo mbioni kuachana na klabu yake ya Al Hilal Fc ya nchini Saudi Arabia kwa makubaliano ya pande mbili kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Fowadi huyo supastaa alihamia kwenye Saudi Pro League akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2023 na alisaini mkataba uliokuwa ukimshuhudia akilipwa Pauni 2.5 milioni kwa wiki katika klabu hiyo ya Al Hilal inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Pamoja na kulipwa mabilioni hayo bahati mbaya kwa Mshambuliaji  huyo amekuwa akiandamwa na majeraha mengi, ikiwamo tatizo la goti lililomfanya awe nje kwa msimu mzima wa 2023-24.

banner

Tangu asajiliwe na klabu hiyo Mshambuliaji huyo amefunga bao moja na asisti tatu katika mechi saba alizocheza kwa kipindi cha miaka miwili huko Kingdom Arena na hilo ni moja ya sababu iliyofanya staa huyo wa zamani wa Barcelona kufikia maku-baliano ya kusitisha mkataba wake Al Hilal, ambayo ilitangaza kuachana na mchezaji huyo.

“Al Hilal na Neymar wamekubaliana kusitisha mkataba kwa makubaliano ya pande mbili”,Ilisomeka taarifa ya klabu hiyo ambayo iliendelea  “Klabu inamshukuru sana Neymar kwa kile alichokifanya kwa kipindi chake alichokuwa Al Hilal na tunamtakia mafanikio mema kwenye maisha yake ya soka”,Ilimalizia kusema taarifa hiyo.

Neymar aling’ara katika klabu za Santos na Barcelona kisha Paris St.German lakini tangu atue Uarabuni amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na matatizo hayo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited