Tetesi zinaeleza kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Sc,Mrisho Ngassa yupo kwenye rada za kutua Kitayosce Fc ambayo inajiandaa kushiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Ngassa aliyewahi kucheza ndani ya Kagera Sugar,Azam Fc,Simba ,Ndanda na Mbeya City amemaliza msimu akiwa na mabao manne huko Jangwani.
Mshambuliaji huyo hakufanikiwa kuongezewa mkataba na mabosi wa Yanga Sc kutokana na kutokuwepo kwenye mpango wa msimu ujao wa ligi kuu bara ,licha ya kuwa na mapenzi mengi na klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.