Mwenyekiti wa klabu ya Simba sc, Murtaza Mangungu amesema ahadi aliyotoa kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya kuifunga Yanga itaendelea kwa miaka minne mpaka atakapoondoka madarakani.
Mangungu amesema watu wengi wakiwemo mashabiki wa Yanga sc walimponda na kumbeza kuhusu kauli yake hiyo lakini athari yake imeonekana baada ya kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Wakati natoa ahadi ile sikuwa na bahatisha, nilikuwa na uhakika na timu yangu na Yanga wanatakiwa kujua kwamba pale siyo mwisho tutaendelea kuwafunga hadi niondoke madarakani, ndio ahadi inaisha”.Amesema Mangungu.
Mangungu anatarajiwa kuiongoza Simba sc hadi Januari 2026 kipindi ambacho uongozi wake utafika kikomo baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika miezi michache mwanzoni mwa mwaka huu.