Haruna Niyonzima ambaye ni kiungo katika timu ya wananchi Yanga Sc amekiongoza kikosi chake kutinga robo fainali baada ya kufunga bao 1-0 dhidi ya Gwambina katika uwanja wa Uhuru.
Bao la ushindi lilifungwa dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko kwa shuti kali alilopiga Niyonzima akiwa nje ya 18.
Uimara wa mlinda mlango wa Yanga Metacha Mnata umesaidia kipindi cha pili cha mchezo Gwambina Fc kushindwa kurudisha bao na ushindi kubakia Yanga.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.