Home Soka Novatus Aondoka Shakhtar

Novatus Aondoka Shakhtar

by Sports Leo
0 comments

Novatus Dismas Miroshi, rasmi ametambulishwa na timu ya Goztepe inayoshiriki Ligi kuu nchini Uturuki kwa mkataba wa miaka minne akitokea Shaktar Donetsk alipokuwa kwa mkopo wa msimu mzima.

Kiungo huyo mtanzania ambaye pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto ama wa kati alijiunga na Shakhtar Donestsk ya nchini Ukraine kwa mkopo wa msimu mzima akitokea klabu ya SV Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Baada ya kutua Shakhtar kiungo alianza vizuri lakini baadae alianza kuwekwa benchi huku kocha Marino Pusic alipendelea zaidi kumtumia Valeriy Bondar na Mykola Matviienko kati ya mabeki wake wa kati huku kushoto akicheza Irakli Azarovi maeneo ambayo Novatus amekuwa akiyamudu.

banner

Licha ya mkataba wake na Zulte kumalizika Juni 2025 staa huyo aliamua kuondoka baada ya kupata dili hilo la nchini Ubelgiji ambapo atakaa mpaka mwaka 2028 baada ya kusaini Mkataba wa miaka minne.

Novatus kabla ya kuondoka nchini alianza kucheza katika klabu ya Azam Fc kisha akajiunga na timu ya Biashara United na baada ya hapo akapata dili nchini Israel ambapo ndipo neema ilipofunguka na kwenda barani ulaya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited