Kocha mkuu wa Chelsea ,Frank Lampard aliyewahi kukichezea kikosi hicho hapo awali kwa kufundishwa na Jose Mourinho ambaye ni kocha mkuu wa Spurs amesema kuwa mpango wake kwa sasa ni kuwauza nyota wake nane ndani ya kikosi hicho.
Japokuwa Mourinho amekuwa ndiye mwalimu kwa Lampard amepigwa nje ndani na mwanafunzi wake kwenye mechi kadhaa za ligi walipokutana.
Miongoni mwa wachezaji ambao Lampard amepanga kuwauza msimu huu ni Kepa Arrizabalaga,Ross Barkley na Jorginho.
Wengine ni wale walioshindwa kutimiza majukumu yao ndani ya kikosi ambao ni Marcos Alonso, Emerson, Kurt Zouma, Willian na Pedro.