Home Makala Okrah Aiponza Yanga Sc

Okrah Aiponza Yanga Sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Shirikisho la soka Duniani (Fifa) limeitwanga barua klabu ya Yanga sc kukamilisha malipo ya ununuzi wa mchezaji Augustine Okrah inayodaiwa na klabu yake ya zamani Benchem United ya nchini Ghana.

Katika barua hiyo inaeleza kuwa Shirikisho hilo lilipokea malalamiko kutoka Benchem kuwa Yanga sc haijakamilisha malipo ya usajili wa staa huyo ambapo makubaliano yalikua kulipa kiasi cha dola laki moja lakini klabu hiyo ililipa dola elfu arobaini pekee huku ikiahidi kumalizia kiasi kilichobaki ndani ya muda mfupi.

banner

Kutokana na tayari mchezaji huyo alishaondoka Yanga sc huku kiasi hicho kukiwa hakijalipwa mpaka sasa Benchem United ilifungua madam Fifa ikiomba fedha hizo kiasi cha dola elfu themanini ambazo ni takribani milioni 216 zilipwe mpaka kufikia Septemba.

Yanga sc wametumiwa uamuzi huo na Fifa huku wakitakiwa kukubali ama kukataa kulipa fedha hizo na mwisho wa kujibu ni Septemba 3 mwaka huu na wasipojibu basi itafahamika kama wamekubaliana na hukumu hiyo.

Mpaka sasa kwa upande wa klabu bado haijatoa majibu kuhusu hatua ambazo watazichukua kuhusu uamuzi huo wa Fifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited