Home Makala Onyango Azua Balaa Simba sc

Onyango Azua Balaa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kati wa Simba, Joash Onyango amegomea kwenda nchini Sudan kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan ili kujiweka sawa na michuano ya kimataifa inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Inaelezwa kuwa raia huyo wa Kenya alikuwa katika orodha ya nyota waliotakiwa kusafiri ikiwemo kupata visa na tiketi ya ndege, lakini baada ya mazoezi ya mwisho kumalizika aligomea kwenda nchini humokushiriki katika michuano hiyo ya michezo miwili ya kirafiki.

Onyango inaelezwa aliwambia Kocha Zoran Maki pamoja na meneja wa timu hiyo Rweyemamu kuwa hapendezewi na suala la kuwekwa benchi kama ilivyokuwa katika mechi tatu za kimashindano zilizopita pamoja na baadhi ya stahiki zake za msingi kutokupatiwa hadi leo na uongozi kama walivyokubaliana katika mkataba mpya.

banner

Mpaka sasa uongozi wa klabu ya Simba sc haujatoa msimamo wao kama watamuuza ama watakubaliana na matakwa ya mchezaji huyo ya kuvunja mkataba wake ili awe huru kutafuta timu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited