Taarifa kutoka Nchini Kenya zimethibitisha kuwa Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba sc Joash Onyango anaweza kutimka klabuni kabla ya mechi za mwisho wa msimu huu kumalizika kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi
Inafahamika kuwa beki huyo hana tena moyo wa kuitumikia klabu hiyo na upo uwezekano asimalizie hata Michezo iliyosalia ya Ligi kuu huku pia akikosa ligi ya Supercup inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwamwezi wa nane mwaka huu ambapo Simba sc ni mshiriki pekee katika michuano hiyo kutoka Afrika mashariki.
Za chini ya kapeti zinasema kwa beki huyo raia wa Kenya huenda akatimkia Afrika Kusini licha ya vilabu baadhi kutoka nchini Kenya ikiwapo Klabu yake ya Zamani ya Gormahia Fc kuonyesha nia ya kumrejesha tena.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bado sababu ya Joash kutohitaji kuendelea kusalia Simba Sc hazijafahamika lakini taarifa za ndani zinasema kuwa beki huyo ana tatizo la kisaikolojia hasa baada ya kuona kiwango chake kimeshuka kiasi cha kusababisha magoli hasa katika mchezo dhidi ya Raja Casablanca na dhidi ya Azam Fc hivyo anaona ni bora atafute sehemu nyingine kwenda kurejesha uwezo wake maana imani ya mashabiki dhidi yake imeshuka maradufu.