Mchezaji wa Simba SC, Mohamed Ouattara amerejea katika viwanja vya mazoezi baada ya kukaa nje kwa miezi kidhaa akisumbuliwa na majeraha na kukosa michezo kadhaa ya ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Ouattara ameanza mazoezi mepesi chini ya Kocha wa Viungo, Kelvin Mandla kwaajili ya kuweka mwili sawa kuelekea mechi mbili za NBC Premier League zilizosalia kukamilisha msimu wa 2022/2023.
Beki huyo tangu amesajiliwa amekosa namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo akiwaacha Joash Onyango na Henock Inonga wakianza katika michezo lukuki ya ligi kuu na kimataifa huku pia kukiwa na taarifa za staa huyo kutemwa msimu huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ouattara alijiunga na Simba sc akitokea Al Hilal Fc ya Sudan ambapo alikua anapata nafasi ya mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na lakini mambo yamekua magumu kwake tangu atue msimbazi.