Klabu ya Yanga imenogewa na biashara na wachezaji kutoka DR Congo na sasa iko kwenye hatua za mwisho kumsaini winga fundi kutoka Union Maniema, Basiala Agee (25) ambaye alikua ni pacha wa Maxi Nzengeli klabuni hapo.
Kwenye Ligi ya Congo sasa Basiala amefanikiwa kufunga mabao matano na kutoa asisti tano huku akiwa amekosa mechi mbili za mwisho kutokana na maaamuzi viongozi wakijiandaa kumruhusu aondoke kuanza maisha mapya na Mabingwa wa nchi, Yanga SC.
Inasemekana kuwa usajili wa staa huyo unakuja kuchukua nafasi ya Jesus Moloko ambaye kocha Miguel Gamond hajaridhika na ufanisi wake hivyo anaona ni bora apishe usajili mpya katika nafasi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa Yanga sc imemtambulisha Shekhan Hamis kiungo iliyemsajili kutoka Jku ya Zanzibar ikiwa ni usajili wake wa kwanza katika dirisha dogo la usajili.