Home Makala Petr Cech Atua Chelsea Kama Mshauri

Petr Cech Atua Chelsea Kama Mshauri

by Sports Leo
0 comments

Aliyekuwa kipa wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Petr Cech amerejea kwenye timu yake ya zamani Chelsea (The Blues) kama mshauri wa masuala ya ufundi kwa makipa.

Petr mwenye umri wa miaka 34 ameteuliwa na Lampard ambaye ni kocha mkuu wa kikosi hicho cha The Blues akiwa amevutiwa na rekodi za hapo awali alipokuwa ndani ya uwanja.

Kiongozi wa Chelsea ,Marina Granovskaia amefurahi kuona Petr amerejea nyumbani kwani anaamini watafikia malengo ambayo wanahitaji kwa kuwa watapata kile ambacho anacho kwa manufaa ya timu kiujumla.

Pia Cech ameorodheshwa kwenye majina ya makocha ambapo ikitokea dharula anaweza kuanza kikosi cha kwanza ndani ya ligi kuu England pamoja na mashindano mengine.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited